Al-Alaq

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ
2 Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ
3 Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ
4 Ambaye amefundisha kwa kalamu. الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ
5 Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ
6 Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَى
7 Akijiona katajirika. أَن رَّآهُ اسْتَغْنَى
8 Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. إِنَّ إِلَى رَبِّكَ الرُّجْعَى
9 Umemwona yule anaye mkataza أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَى
10 Mja anapo sali? عَبْدًا إِذَا صَلَّى
11 Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَى
12 Au anaamrisha uchamngu? أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَى
13 Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّى
14 Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? أَلَمْ يَعْلَمْ بِأَنَّ اللَّهَ يَرَى
15 Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ
16 Shungi la uwongo, lenye makosa! نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ
17 Basi na awaite wenzake! فَلْيَدْعُ نَادِيَه
18 Nasi tutawaita Mazabania! سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ
19 Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِبْ
;