At-Tin

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa tini na zaituni! وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ
2 Na kwa Mlima wa Sinai! وَطُورِ سِينِينَ
3 Na kwa mji huu wenye amani! وَهَذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ
4 Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ
5 Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ
6 Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ
7 Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ
8 Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? أَلَيْسَ اللَّهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ
;