Adh-Dhuha

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa mchana! وَالضُّحَى
2 Na kwa usiku unapo tanda! وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَى
3 Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَى
4 Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَى
5 Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَى
6 Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَى
7 Na akakukuta umepotea akakuongoa? وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَى
8 Akakukuta mhitaji akakutosheleza? وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَى
9 Basi yatima usimwonee! فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ
10 Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ
11 Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ
;