Al-A'la

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa, سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
2 Aliye umba, na akaweka sawa, الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّى
3 Na ambaye amekadiria na akaongoa, وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَى
4 Na aliye otesha malisho, وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَى
5 Kisha akayafanya makavu, meusi. فَجَعَلَهُ غُثَاء أَحْوَى
6 Tutakusomesha wala hutasahau, سَنُقْرِؤُكَ فَلَا تَنسَى
7 Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. إِلَّا مَا شَاء اللَّهُ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَى
8 Na tutakusahilishia yawe mepesi. وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَى
9 Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَى
10 Atakumbuka mwenye kuogopa. سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَى
11 Na atajitenga mbali nayo mpotovu, وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى
12 Ambaye atauingia Moto mkubwa. الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَى
13 Tena humo hatakufa wala hawi hai. ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَى
14 Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّى
15 Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّى
16 Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
17 Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَى
18 Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, إِنَّ هَذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَى
19 Vitabu vya Ibrahimu na Musa. صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى
;