Al-Gashiya

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
2 Siku hiyo nyuso zitainama, وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ
3 Zikifanya kazi, nazo taabani. عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ
4 Ziingie katika Moto unao waka - تَصْلَى نَارًا حَامِيَةً
5 Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. تُسْقَى مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ
6 Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ
7 Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. لَا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ
8 Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ
9 Zitakuwa radhi kwa juhudi yao, لِسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ
10 Katika Bustani ya juu. فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ
11 Hawatasikia humo upuuzi. لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً
12 Humo imo chemchem inayo miminika. فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ
13 Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ
14 Na bilauri zilizo pangwa, وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ
15 Na matakia safu safu, وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ
16 Na mazulia yaliyo tandikwa. وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ
17 Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ
18 Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? وَإِلَى السَّمَاء كَيْفَ رُفِعَتْ
19 Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ
20 Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ
21 Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ
22 Wewe si mwenye kuwatawalia. لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ
23 Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, إِلَّا مَن تَوَلَّى وَكَفَرَ
24 Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa! فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ
25 Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ
26 Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao! ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُمْ
;