At-Tariq

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! وَالسَّمَاء وَالطَّارِقِ
2 Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ
3 Ni Nyota yenye mwanga mkali. النَّجْمُ الثَّاقِبُ
4 Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ
5 Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ
6 Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, خُلِقَ مِن مَّاء دَافِقٍ
7 Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ
8 Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. إِنَّهُ عَلَى رَجْعِهِ لَقَادِرٌ
9 Siku zitakapo dhihirishwa siri. يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ
10 Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ
11 Naapa kwa mbingu yenye marejeo! وَالسَّمَاء ذَاتِ الرَّجْعِ
12 Na kwa ardhi inayo pasuka! وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ
13 Hakika hii ni kauli ya kupambanua. إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ
14 Wala si mzaha. وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ
15 Hakika wao wanapanga mpango. إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا
16 Na Mimi napanga mpango. وَأَكِيدُ كَيْدًا
17 Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا
;