Abasa

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Alikunja kipaji na akageuka, عَبَسَ وَتَوَلَّى
2 Kwa sababu alimjia kipofu! أَن جَاءهُ الْأَعْمَى
3 Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّى
4 Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَى
5 Ama ajionaye hana haja, أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَى
6 Wewe ndio unamshughulikia? فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّى
7 Na si juu yako kama hakutakasika. وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّى
8 Ama anaye kujia kwa juhudi, وَأَمَّا مَن جَاءكَ يَسْعَى
9 Naye anaogopa, وَهُوَ يَخْشَى
10 Ndio wewe unampuuza? فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّى
11 Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ
12 Basi anaye penda akumbuke. فَمَن شَاء ذَكَرَهُ
13 Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ
14 Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ
15 Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, بِأَيْدِي سَفَرَةٍ
16 Watukufu, wema. كِرَامٍ بَرَرَةٍ
17 Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ
18 Kwa kitu gani amemuumba? مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ
19 Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ
20 Kisha akamsahilishia njia. ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ
21 Kisha akamfisha, akamtia kaburini. ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ
22 Kisha apendapo atamfufua. ثُمَّ إِذَا شَاء أَنشَرَهُ
23 La! Hajamaliza aliyo muamuru. كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ
24 Hebu mtu na atazame chakula chake. فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَى طَعَامِهِ
25 Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاء صَبًّا
26 Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا
27 Kisha tukaotesha humo nafaka, فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا
28 Na zabibu, na mimea ya majani, وَعِنَبًا وَقَضْبًا
29 Na mizaituni, na mitende, وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا
30 Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, وَحَدَائِقَ غُلْبًا
31 Na matunda, na malisho ya wanyama; وَفَاكِهَةً وَأَبًّا
32 Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ
33 Basi utakapo kuja ukelele, فَإِذَا جَاءتِ الصَّاخَّةُ
34 Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ
35 Na mamaye na babaye, وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ
36 Na mkewe na wanawe - وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ
37 Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ
38 Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ
39 Zitacheka, zitachangamka; ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ
40 Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ
41 Giza totoro litazifunika, تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ
42 Hao ndio makafiri watenda maovu. أُوْلَئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ
;