At-Takwir

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Jua litakapo kunjwa, إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ
2 Na nyota zikazimwa, وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ
3 Na milima ikaondolewa, وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ
4 Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ
5 Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ
6 Na bahari zikawaka moto, وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ
7 Na nafsi zikaunganishwa, وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ
8 Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, وَإِذَا الْمَوْؤُودَةُ سُئِلَتْ
9 Kwa kosa gani aliuliwa? بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ
10 Na madaftari yatakapo enezwa, وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ
11 Na mbingu itapo tanduliwa, وَإِذَا السَّمَاء كُشِطَتْ
12 Na Jahannamu itapo chochewa, وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ
13 Na Pepo ikasogezwa, وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ
14 Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ
15 Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ
16 Zinazo kwenda, kisha zikajificha, الْجَوَارِ الْكُنَّسِ
17 Na kwa usiku unapo pungua, وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ
18 Na kwa asubuhi inapo pambazuka, وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ
19 Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ
20 Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ
21 Anaye t'iiwa, tena muaminifu. مُطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ
22 Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ
23 Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ
24 Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ
25 Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَجِيمٍ
26 Basi mnakwenda wapi? فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ
27 Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ
28 Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. لِمَن شَاء مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ
29 Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. وَمَا تَشَاؤُونَ إِلَّا أَن يَشَاء اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
;