An-Nazi'at

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu, وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا
2 Na kwa wanao toa kwa upole, وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا
3 Na wanao ogelea, وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا
4 Wakishindana mbio, فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا
5 Wakidabiri mambo. فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا
6 Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka, يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ
7 Kifuate cha kufuatia. تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ
8 Siku hiyo nyoyo zitapiga piga, قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ
9 Macho yatainama chini. أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ
10 Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? يَقُولُونَ أَئِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ
11 Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? أَئِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً
12 Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ
13 Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ
14 Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ
15 Je! Imekufikia hadithi ya Musa? هَلْ أتَاكَ حَدِيثُ مُوسَى
16 Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى
17 Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. اذْهَبْ إِلَى فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَى
18 Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَى أَن تَزَكَّى
19 Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. وَأَهْدِيَكَ إِلَى رَبِّكَ فَتَخْشَى
20 Basi alimwonyesha Ishara kubwa. فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَى
21 Lakini aliikadhibisha na akaasi. فَكَذَّبَ وَعَصَى
22 Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَى
23 Akakusanya watu akanadi. فَحَشَرَ فَنَادَى
24 Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَى
25 Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَى
26 Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. إِنَّ فِي ذَلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَى
27 Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاء بَنَاهَا
28 Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا
29 Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا
30 Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَلِكَ دَحَاهَا
31 Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءهَا وَمَرْعَاهَا
32 Na milima akaisimamisha, وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا
33 Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ
34 Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, فَإِذَا جَاءتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَى
35 Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَى
36 Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَى
37 Basi ama yule aliye zidi ujeuri, فَأَمَّا مَن طَغَى
38 Na akakhiari maisha ya dunia, وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
39 Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَى
40 Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَى
41 Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَى
42 Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا
43 Una nini wewe hata uitaje? فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا
44 Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. إِلَى رَبِّكَ مُنتَهَاهَا
45 Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا
46 Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا
;