An-Nabaa

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 WANAULIZANA nini? عَمَّ يَتَسَاءلُونَ
2 Ile khabari kuu, عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ
3 Ambayo kwayo wanakhitalifiana. الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ
4 La! Karibu watakuja jua. كَلَّا سَيَعْلَمُونَ
5 Tena la! Karibu watakuja jua. ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ
6 Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا
7 Na milima kama vigingi? وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا
8 Na tukakuumbeni kwa jozi? وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا
9 Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا
10 Na tukaufanya usiku ni nguo? وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا
11 Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا
12 Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا
13 Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا
14 Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاء ثَجَّاجًا
15 Ili tutoe kwayo nafaka na mimea, لِنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا
16 Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا
17 Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا
18 Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا
19 Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango, وَفُتِحَتِ السَّمَاء فَكَانَتْ أَبْوَابًا
20 Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا
21 Hakika Jahannamu inangojea! إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا
22 Kwa walio asi ndio makaazi yao, لِلْطَّاغِينَ مَآبًا
23 Wakae humo karne baada ya karne, لَابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا
24 Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا
25 Ila maji yamoto sana na usaha, إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا
26 Ndio jaza muwafaka. جَزَاء وِفَاقًا
27 Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا
28 Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا
29 Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا
30 Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا
31 Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا
32 Mabustani na mizabibu, حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا
33 Na wake walio lingana nao, وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا
34 Na bilauri zilizo jaa, وَكَأْسًا دِهَاقًا
35 Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo - لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا
36 Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. جَزَاء مِّن رَّبِّكَ عَطَاء حِسَابًا
37 Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرحْمَنِ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا
38 Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرحْمَنُ وَقَالَ صَوَابًا
39 Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi. ذَلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ فَمَن شَاء اتَّخَذَ إِلَى رَبِّهِ مَآبًا
40 Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا
;