Al-Mursalat

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا
2 Na zinazo vuma kwa kasi! فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا
3 Na zikaeneza maeneo yote! وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا
4 Na zinazo farikisha zikatawanya! فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا
5 Na zinazo peleka mawaidha! فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا
6 Kwa kuudhuru au kuonya, عُذْرًا أَوْ نُذْرًا
7 Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ
8 Wakati nyota zitakapo futwa, فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ
9 Na mbingu zitakapo pasuliwa, وَإِذَا السَّمَاء فُرِجَتْ
10 Na milima itakapo peperushwa, وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ
11 Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ
12 Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ
13 Kwa siku ya kupambanua! لِيَوْمِ الْفَصْلِ
14 Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ
15 Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
16 Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ
17 Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ
18 Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! كَذَلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ
19 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
20 Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاء مَّهِينٍ
21 Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ
22 Mpaka muda maalumu? إِلَى قَدَرٍ مَّعْلُومٍ
23 Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ
24 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
25 Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا
26 Walio hai na maiti? أَحْيَاء وَأَمْوَاتًا
27 Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاء فُرَاتًا
28 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
29 Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! انطَلِقُوا إِلَى مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ
30 Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! انطَلِقُوا إِلَى ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ
31 Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. لَا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ
32 Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ
33 Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ
34 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
35 Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, هَذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ
36 Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ
37 Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
38 Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. هَذَا يَوْمُ الْفَصْلِ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ
39 Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ
40 Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
41 Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ
42 Na matunda wanayo yapenda, وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ
43 Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
44 Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنينَ
45 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
46 Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ
47 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
48 Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ
49 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
50 Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ
;