Az-Zariyat

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa pepo zinazo tawanya, وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا
2 Na zinazo beba mizigo, فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا
3 Na zinazo kwenda kwa wepesi. فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا
4 Na zinazo gawanya kwa amri, فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا
5 Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli, إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ
6 Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ
7 Naapa kwa mbingu zenye njia, وَالسَّمَاء ذَاتِ الْحُبُكِ
8 Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ
9 Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ
10 Wazushi wameangamizwa. قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ
11 Ambao wameghafilika katika ujinga. الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ
12 Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ
13 Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ
14 Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ
15 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
16 Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُحْسِنِينَ
17 Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ
18 Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
19 Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ
20 Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ
21 Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? وَفِي أَنفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
22 Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. وَفِي السَّمَاء رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ
23 Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. فَوَرَبِّ السَّمَاء وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
24 Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ
25 Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
26 Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. فَرَاغَ إِلَى أَهْلِهِ فَجَاء بِعِجْلٍ سَمِينٍ
27 Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
28 Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً قَالُوا لَا تَخَفْ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ
29 Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ
30 Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. قَالُوا كَذَلِكَ قَالَ رَبُّكِ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ
31 AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
32 Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
33 Tuwatupie mawe ya udongo, لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ
34 Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. مُسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ
35 Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
36 Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ الْمُسْلِمِينَ
37 Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ
38 Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. وَفِي مُوسَى إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَى فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
39 Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! فَتَوَلَّى بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
40 Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ
41 Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ
42 Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. مَا تَذَرُ مِن شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ
43 Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّى حِينٍ
44 Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ
45 Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. فَمَا اسْتَطَاعُوا مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ
46 Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ
47 Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. وَالسَّمَاء بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
48 Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ
49 Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. وَمِن كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
50 Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
51 Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
52 Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. كَذَلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
53 Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. أَتَوَاصَوْا بِهِ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
54 Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ
55 Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ
56 Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
57 Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe. مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ
58 Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ
59 Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ
60 Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
;