1 |
Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu! |
/content/ayah/audio/hudhaify/050001.mp3
|
ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ |
2 |
Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu! |
/content/ayah/audio/hudhaify/050002.mp3
|
بَلْ عَجِبُوا أَن جَاءهُمْ مُنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ الْكَافِرُونَ هَذَا شَيْءٌ عَجِيبٌ |
3 |
Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali! |
/content/ayah/audio/hudhaify/050003.mp3
|
أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ذَلِكَ رَجْعٌ بَعِيدٌ |
4 |
Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050004.mp3
|
قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ الْأَرْضُ مِنْهُمْ وَعِندَنَا كِتَابٌ حَفِيظٌ |
5 |
Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050005.mp3
|
بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءهُمْ فَهُمْ فِي أَمْرٍ مَّرِيجٍ |
6 |
Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050006.mp3
|
أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاء فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ |
7 |
Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050007.mp3
|
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ |
8 |
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050008.mp3
|
تَبْصِرَةً وَذِكْرَى لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ |
9 |
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050009.mp3
|
وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاء مَاء مُّبَارَكًا فَأَنبَتْنَا بِهِ جَنَّاتٍ وَحَبَّ الْحَصِيدِ |
10 |
Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi, |
/content/ayah/audio/hudhaify/050010.mp3
|
وَالنَّخْلَ بَاسِقَاتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ |
11 |
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050011.mp3
|
رِزْقًا لِّلْعِبَادِ وَأَحْيَيْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا كَذَلِكَ الْخُرُوجُ |
12 |
Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050012.mp3
|
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَابُ الرَّسِّ وَثَمُودُ |
13 |
Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050013.mp3
|
وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَانُ لُوطٍ |
14 |
Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050014.mp3
|
وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ كُلٌّ كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ |
15 |
Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050015.mp3
|
أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الْأَوَّلِ بَلْ هُمْ فِي لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ |
16 |
Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050016.mp3
|
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ |
17 |
Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050017.mp3
|
إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ |
18 |
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050018.mp3
|
مَا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ |
19 |
Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050019.mp3
|
وَجَاءتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ذَلِكَ مَا كُنتَ مِنْهُ تَحِيدُ |
20 |
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050020.mp3
|
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ ذَلِكَ يَوْمُ الْوَعِيدِ |
21 |
Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050021.mp3
|
وَجَاءتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّعَهَا سَائِقٌ وَشَهِيدٌ |
22 |
(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050022.mp3
|
لَقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ |
23 |
Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050023.mp3
|
وَقَالَ قَرِينُهُ هَذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ |
24 |
Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda, |
/content/ayah/audio/hudhaify/050024.mp3
|
أَلْقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ |
25 |
Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka, |
/content/ayah/audio/hudhaify/050025.mp3
|
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ |
26 |
Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050026.mp3
|
الَّذِي جَعَلَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِي الْعَذَابِ الشَّدِيدِ |
27 |
Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050027.mp3
|
قَالَ قَرِينُهُ رَبَّنَا مَا أَطْغَيْتُهُ وَلَكِن كَانَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ |
28 |
(Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050028.mp3
|
قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِالْوَعِيدِ |
29 |
Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050029.mp3
|
مَا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ وَمَا أَنَا بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ |
30 |
Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada? |
/content/ayah/audio/hudhaify/050030.mp3
|
يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ |
31 |
Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050031.mp3
|
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ |
32 |
Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050032.mp3
|
هَذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ |
33 |
Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio elekea- |
/content/ayah/audio/hudhaify/050033.mp3
|
مَنْ خَشِيَ الرَّحْمَن بِالْغَيْبِ وَجَاء بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ |
34 |
(Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050034.mp3
|
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ ذَلِكَ يَوْمُ الْخُلُودِ |
35 |
Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050035.mp3
|
لَهُم مَّا يَشَاؤُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ |
36 |
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia? |
/content/ayah/audio/hudhaify/050036.mp3
|
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا فَنَقَّبُوا فِي الْبِلَادِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ |
37 |
Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050037.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ |
38 |
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050038.mp3
|
وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ |
39 |
Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050039.mp3
|
فَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ |
40 |
Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050040.mp3
|
وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ |
41 |
Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050041.mp3
|
وَاسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ |
42 |
Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050042.mp3
|
يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ذَلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ |
43 |
Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050043.mp3
|
إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا الْمَصِيرُ |
44 |
Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050044.mp3
|
يَوْمَ تَشَقَّقُ الْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ذَلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ |
45 |
Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/050045.mp3
|
نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ |