Ash-Shams

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Naapa kwa jua na mwangaza wake! وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا
2 Na kwa mwezi unapo lifuatia! وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا
3 Na kwa mchana unapo lidhihirisha! وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا
4 Na kwa usiku unapo lifunika! وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا
5 Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! وَالسَّمَاء وَمَا بَنَاهَا
6 Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا
7 Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا
8 Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا
9 Hakika amefanikiwa aliye itakasa, قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا
10 Na hakika amekhasiri aliye iviza. وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا
11 Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا
12 Alipo simama mwovu wao mkubwa, إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا
13 Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ نَاقَةَ اللَّهِ وَسُقْيَاهَا
14 Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا
15 Wala Yeye haogopi matokeo yake. وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا
;