Al-Inshiqaq

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Itapo chanika mbingu, إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ
2 Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
3 Na ardhi itakapo tanuliwa, وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ
4 Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu, وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ
5 Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
6 Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَى رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ
7 Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia, فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ
8 Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi, فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا
9 Na arudi kwa ahali zake na furaha. وَيَنقَلِبُ إِلَى أَهْلِهِ مَسْرُورًا
10 Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاء ظَهْرِهِ
11 Basi huyo ataomba kuteketea. فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا
12 Na ataingia Motoni. وَيَصْلَى سَعِيرًا
13 Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا
14 Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ
15 Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! بَلَى إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا
16 Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa, فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ
17 Na kwa usiku na unavyo vikusanya, وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ
18 Na kwa mwezi unapo pevuka, وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ
19 Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka! لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ
20 Basi wana nini hawaamini? فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
21 Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu? وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ
22 Bali walio kufuru wanakanusha tu. بَلِ الَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ
23 Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria. وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ
24 Basi wabashirie adhabu chungu! فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
25 Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. إِلَّا الَّذِينَ آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ
;