Al-Ma'arij

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ
2 Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - لِّلْكَافِرينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ
3 Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. مِّنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ
4 Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ
5 Basi subiri kwa subira njema. فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا
6 Hakika wao wanaiona iko mbali, إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا
7 Na Sisi tunaiona iko karibu. وَنَرَاهُ قَرِيبًا
8 Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاء كَالْمُهْلِ
9 Na milima itakuwa kama sufi. وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ
10 Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا
11 Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, يُبَصَّرُونَهُمْ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ
12 Na mkewe, na nduguye, وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ
13 Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْويهِ
14 Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ
15 La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, كَلَّا إِنَّهَا لَظَى
16 Unao babua ngozi ya kichwa! نَزَّاعَةً لِّلشَّوَى
17 Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّى
18 Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. وَجَمَعَ فَأَوْعَى
19 Hakika mtu ameumbwa na papara. إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا
20 Inapo mgusa shari hupapatika. إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا
21 Na inapo mgusa kheri huizuilia. وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا
22 Isipo kuwa wanao sali, إِلَّا الْمُصَلِّينَ
23 Ambao wanadumisha Sala zao, الَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ
24 Na ambao katika mali yao iko haki maalumu وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ
25 Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ
26 Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ
27 Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ
28 Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ
29 Na ambao wanahifadhi tupu zao. وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ
30 Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
31 Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاء ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ
32 Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ
33 Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ
34 Na ambao wanazihifadhi Sala zao. وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
35 Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. أُوْلَئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ
36 Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ
37 Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ
38 Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ
39 La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. كَلَّا إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ
40 Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ
41 Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. عَلَى أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
42 Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّى يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
43 Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَى نُصُبٍ يُوفِضُونَ
44 Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ذَلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ
;