1 |
T'aa Siin Miim. (T'. S. M.) |
/content/ayah/audio/hudhaify/026001.mp3
|
طسم |
2 |
Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026002.mp3
|
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ |
3 |
Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026003.mp3
|
لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ |
4 |
Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026004.mp3
|
إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّن السَّمَاء آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ |
5 |
Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026005.mp3
|
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ الرَّحْمَنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ |
6 |
Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026006.mp3
|
فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنبَاء مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُون |
7 |
Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026007.mp3
|
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ |
8 |
Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026008.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
9 |
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026009.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
10 |
Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026010.mp3
|
وَإِذْ نَادَى رَبُّكَ مُوسَى أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ |
11 |
Watu wa Firauni. Hawaogopi? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026011.mp3
|
قَوْمَ فِرْعَوْنَ أَلَا يَتَّقُونَ |
12 |
Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026012.mp3
|
قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ |
13 |
Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026013.mp3
|
وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَى هَارُونَ |
14 |
Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026014.mp3
|
وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ |
15 |
Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026015.mp3
|
قَالَ كَلَّا فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ |
16 |
Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026016.mp3
|
فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ |
17 |
Waachilie Wana wa Israili wende nasi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026017.mp3
|
أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ |
18 |
(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026018.mp3
|
قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ |
19 |
Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026019.mp3
|
وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ |
20 |
(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026020.mp3
|
قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ |
21 |
Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026021.mp3
|
فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكْمًا وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُرْسَلِينَ |
22 |
Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026022.mp3
|
وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ |
23 |
Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026023.mp3
|
قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ |
24 |
Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026024.mp3
|
قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إن كُنتُم مُّوقِنِينَ |
25 |
(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026025.mp3
|
قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ |
26 |
(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026026.mp3
|
قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ |
27 |
(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026027.mp3
|
قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ |
28 |
(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026028.mp3
|
قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ |
29 |
(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026029.mp3
|
قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ |
30 |
Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026030.mp3
|
قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ |
31 |
Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026031.mp3
|
قَالَ فَأْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ |
32 |
Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026032.mp3
|
فَأَلْقَى عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ |
33 |
Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026033.mp3
|
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاء لِلنَّاظِرِينَ |
34 |
(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026034.mp3
|
قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ |
35 |
Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026035.mp3
|
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ |
36 |
Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026036.mp3
|
قَالُوا أَرْجِهِ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ |
37 |
Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026037.mp3
|
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ |
38 |
Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026038.mp3
|
فَجُمِعَ السَّحَرَةُ لِمِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ |
39 |
Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026039.mp3
|
وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ |
40 |
Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026040.mp3
|
لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ السَّحَرَةَ إِن كَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ |
41 |
Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026041.mp3
|
فَلَمَّا جَاء السَّحَرَةُ قَالُوا لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ |
42 |
Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026042.mp3
|
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًا لَّمِنَ الْمُقَرَّبِينَ |
43 |
Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026043.mp3
|
قَالَ لَهُم مُّوسَى أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ |
44 |
Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026044.mp3
|
فَأَلْقَوْا حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ الْغَالِبُونَ |
45 |
Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026045.mp3
|
فَأَلْقَى مُوسَى عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ |
46 |
Hapo wachawi walipinduka wakasujudu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026046.mp3
|
فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ |
47 |
Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026047.mp3
|
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ |
48 |
Mola Mlezi wa Musa na Harun. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026048.mp3
|
رَبِّ مُوسَى وَهَارُونَ |
49 |
(Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026049.mp3
|
قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ |
50 |
Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026050.mp3
|
قَالُوا لَا ضَيْرَ إِنَّا إِلَى رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ |
51 |
Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026051.mp3
|
إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ |
52 |
Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026052.mp3
|
وَأَوْحَيْنَا إِلَى مُوسَى أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ |
53 |
Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026053.mp3
|
فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ |
54 |
(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026054.mp3
|
إِنَّ هَؤُلَاء لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ |
55 |
Nao wanatuudhi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026055.mp3
|
وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَائِظُونَ |
56 |
Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026056.mp3
|
وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَاذِرُونَ |
57 |
Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026057.mp3
|
فَأَخْرَجْنَاهُم مِّن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ |
58 |
Na makhazina, na vyeo vya hishima, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026058.mp3
|
وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ |
59 |
Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026059.mp3
|
كَذَلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا بَنِي إِسْرَائِيلَ |
60 |
Basi wakawafuata lilipo chomoza jua. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026060.mp3
|
فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ |
61 |
Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! |
/content/ayah/audio/hudhaify/026061.mp3
|
فَلَمَّا تَرَاءى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَى إِنَّا لَمُدْرَكُونَ |
62 |
(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! |
/content/ayah/audio/hudhaify/026062.mp3
|
قَالَ كَلَّا إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ |
63 |
Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026063.mp3
|
فَأَوْحَيْنَا إِلَى مُوسَى أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ |
64 |
Na tukawajongeza hapo wale wengine. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026064.mp3
|
وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ |
65 |
Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026065.mp3
|
وَأَنجَيْنَا مُوسَى وَمَن مَّعَهُ أَجْمَعِينَ |
66 |
Kisha tukawazamisha hao wengine. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026066.mp3
|
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ |
67 |
Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026067.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
68 |
Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026068.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
69 |
Na wasomee khabari za Ibrahim. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026069.mp3
|
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَاهِيمَ |
70 |
Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026070.mp3
|
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ |
71 |
Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026071.mp3
|
قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ |
72 |
Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026072.mp3
|
قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ |
73 |
Au yanakufaeni, au yanakudhuruni? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026073.mp3
|
أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ |
74 |
Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026074.mp3
|
قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءنَا كَذَلِكَ يَفْعَلُونَ |
75 |
Je! Mmewaona hawa mnao waabudu- |
/content/ayah/audio/hudhaify/026075.mp3
|
قَالَ أَفَرَأَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ |
76 |
Nyinyi na baba zenu wa zamani? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026076.mp3
|
أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمُ الْأَقْدَمُونَ |
77 |
Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026077.mp3
|
فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّي إِلَّا رَبَّ الْعَالَمِينَ |
78 |
Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026078.mp3
|
الَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهْدِينِ |
79 |
Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026079.mp3
|
وَالَّذِي هُوَ يُطْعِمُنِي وَيَسْقِينِ |
80 |
Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026080.mp3
|
وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ |
81 |
Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026081.mp3
|
وَالَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحْيِينِ |
82 |
Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026082.mp3
|
وَالَّذِي أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ |
83 |
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026083.mp3
|
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ |
84 |
Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026084.mp3
|
وَاجْعَل لِّي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الْآخِرِينَ |
85 |
Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026085.mp3
|
وَاجْعَلْنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ |
86 |
Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026086.mp3
|
وَاغْفِرْ لِأَبِي إِنَّهُ كَانَ مِنَ الضَّالِّينَ |
87 |
Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026087.mp3
|
وَلَا تُخْزِنِي يَوْمَ يُبْعَثُونَ |
88 |
Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026088.mp3
|
يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ |
89 |
Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026089.mp3
|
إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ |
90 |
Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026090.mp3
|
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ |
91 |
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026091.mp3
|
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ |
92 |
Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu |
/content/ayah/audio/hudhaify/026092.mp3
|
وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ |
93 |
Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026093.mp3
|
مِن دُونِ اللَّهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ |
94 |
Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026094.mp3
|
فَكُبْكِبُوا فِيهَا هُمْ وَالْغَاوُونَ |
95 |
Na majeshi ya Ibilisi yote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026095.mp3
|
وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ |
96 |
Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo: |
/content/ayah/audio/hudhaify/026096.mp3
|
قَالُوا وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ |
97 |
Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026097.mp3
|
تَاللَّهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ |
98 |
Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026098.mp3
|
إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ |
99 |
Na hawakutupoteza ila wale wakosefu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026099.mp3
|
وَمَا أَضَلَّنَا إِلَّا الْمُجْرِمُونَ |
100 |
Basi hatuna waombezi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026100.mp3
|
فَمَا لَنَا مِن شَافِعِينَ |
101 |
Wala rafiki wa dhati. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026101.mp3
|
وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ |
102 |
Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026102.mp3
|
فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ |
103 |
Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026103.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
104 |
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026104.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
105 |
Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026105.mp3
|
كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ |
106 |
Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026106.mp3
|
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ |
107 |
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026107.mp3
|
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ |
108 |
Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026108.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
109 |
Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026109.mp3
|
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ |
110 |
Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026110.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
111 |
Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026111.mp3
|
قَالُوا أَنُؤْمِنُ لَكَ وَاتَّبَعَكَ الْأَرْذَلُونَ |
112 |
Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026112.mp3
|
قَالَ وَمَا عِلْمِي بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ |
113 |
Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua! |
/content/ayah/audio/hudhaify/026113.mp3
|
إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَى رَبِّي لَوْ تَشْعُرُونَ |
114 |
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026114.mp3
|
وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الْمُؤْمِنِينَ |
115 |
Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026115.mp3
|
إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ |
116 |
Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026116.mp3
|
قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا نُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمَرْجُومِينَ |
117 |
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026117.mp3
|
قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِي كَذَّبُونِ |
118 |
Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026118.mp3
|
فَافْتَحْ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِي مِنَ الْمُؤْمِنِينَ |
119 |
Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026119.mp3
|
فَأَنجَيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ |
120 |
Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026120.mp3
|
ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ الْبَاقِينَ |
121 |
Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026121.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
122 |
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026122.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
123 |
Kina A'd waliwakanusha Mitume. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026123.mp3
|
كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ |
124 |
Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026124.mp3
|
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ |
125 |
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026125.mp3
|
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ |
126 |
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026126.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
127 |
Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026127.mp3
|
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ |
128 |
Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026128.mp3
|
أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ آيَةً تَعْبَثُونَ |
129 |
Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele! |
/content/ayah/audio/hudhaify/026129.mp3
|
وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ |
130 |
Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026130.mp3
|
وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ |
131 |
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026131.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
132 |
Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026132.mp3
|
وَاتَّقُوا الَّذِي أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ |
133 |
Amekupeni wanyama wa kufuga na wana. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026133.mp3
|
أَمَدَّكُم بِأَنْعَامٍ وَبَنِينَ |
134 |
Na mabustani na chemchem. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026134.mp3
|
وَجَنَّاتٍ وَعُيُونٍ |
135 |
Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026135.mp3
|
إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ |
136 |
Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026136.mp3
|
قَالُوا سَوَاء عَلَيْنَا أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ الْوَاعِظِينَ |
137 |
Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026137.mp3
|
إِنْ هَذَا إِلَّا خُلُقُ الْأَوَّلِينَ |
138 |
Wala sisi hatutaadhibiwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026138.mp3
|
وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ |
139 |
Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026139.mp3
|
فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَاهُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
140 |
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026140.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
141 |
Kina Thamud waliwakanusha Mitume. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026141.mp3
|
كَذَّبَتْ ثَمُودُ الْمُرْسَلِينَ |
142 |
Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026142.mp3
|
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَالِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ |
143 |
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026143.mp3
|
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ |
144 |
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026144.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
145 |
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026145.mp3
|
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ |
146 |
Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026146.mp3
|
أَتُتْرَكُونَ فِي مَا هَاهُنَا آمِنِينَ |
147 |
Katika mabustani, na chemchem? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026147.mp3
|
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ |
148 |
Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026148.mp3
|
وَزُرُوعٍ وَنَخْلٍ طَلْعُهَا هَضِيمٌ |
149 |
Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026149.mp3
|
وَتَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا فَارِهِينَ |
150 |
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026150.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
151 |
Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026151.mp3
|
وَلَا تُطِيعُوا أَمْرَ الْمُسْرِفِينَ |
152 |
Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026152.mp3
|
الَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ |
153 |
Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026153.mp3
|
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ |
154 |
Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026154.mp3
|
مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِآيَةٍ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ |
155 |
Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026155.mp3
|
قَالَ هَذِهِ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ |
156 |
Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026156.mp3
|
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ |
157 |
Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026157.mp3
|
فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا نَادِمِينَ |
158 |
Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026158.mp3
|
فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
159 |
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026159.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
160 |
Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026160.mp3
|
كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ الْمُرْسَلِينَ |
161 |
Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026161.mp3
|
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ |
162 |
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026162.mp3
|
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ |
163 |
Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026163.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
164 |
Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026164.mp3
|
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ |
165 |
Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026165.mp3
|
أَتَأْتُونَ الذُّكْرَانَ مِنَ الْعَالَمِينَ |
166 |
Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka! |
/content/ayah/audio/hudhaify/026166.mp3
|
وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُمْ مِنْ أَزْوَاجِكُم بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ |
167 |
Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji! |
/content/ayah/audio/hudhaify/026167.mp3
|
قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا لُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمُخْرَجِينَ |
168 |
Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026168.mp3
|
قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ الْقَالِينَ |
169 |
Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026169.mp3
|
رَبِّ نَجِّنِي وَأَهْلِي مِمَّا يَعْمَلُونَ |
170 |
Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026170.mp3
|
فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ |
171 |
Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026171.mp3
|
إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ |
172 |
Kisha tukawaangamiza wale wengine. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026172.mp3
|
ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ |
173 |
Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026173.mp3
|
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا فَسَاء مَطَرُ الْمُنذَرِينَ |
174 |
Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026174.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
175 |
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026175.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
176 |
Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026176.mp3
|
كَذَّبَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ الْمُرْسَلِينَ |
177 |
Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026177.mp3
|
إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ |
178 |
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026178.mp3
|
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ |
179 |
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026179.mp3
|
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ |
180 |
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026180.mp3
|
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى رَبِّ الْعَالَمِينَ |
181 |
Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026181.mp3
|
أَوْفُوا الْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُخْسِرِينَ |
182 |
Na pimeni kwa haki iliyo nyooka; |
/content/ayah/audio/hudhaify/026182.mp3
|
وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ |
183 |
Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026183.mp3
|
وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ |
184 |
Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026184.mp3
|
وَاتَّقُوا الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالْجِبِلَّةَ الْأَوَّلِينَ |
185 |
Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026185.mp3
|
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ |
186 |
Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026186.mp3
|
وَمَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ |
187 |
Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026187.mp3
|
فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِّنَ السَّمَاء إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ |
188 |
Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026188.mp3
|
قَالَ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ |
189 |
Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026189.mp3
|
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ الظُّلَّةِ إِنَّهُ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ |
190 |
Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026190.mp3
|
إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ |
191 |
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026191.mp3
|
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ |
192 |
Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026192.mp3
|
وَإِنَّهُ لَتَنزِيلُ رَبِّ الْعَالَمِينَ |
193 |
Ameuteremsha Roho muaminifu, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026193.mp3
|
نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ |
194 |
Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026194.mp3
|
عَلَى قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ |
195 |
Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026195.mp3
|
بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ |
196 |
Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026196.mp3
|
وَإِنَّهُ لَفِي زُبُرِ الْأَوَّلِينَ |
197 |
Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026197.mp3
|
أَوَلَمْ يَكُن لَّهُمْ آيَةً أَن يَعْلَمَهُ عُلَمَاء بَنِي إِسْرَائِيلَ |
198 |
Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026198.mp3
|
وَلَوْ نَزَّلْنَاهُ عَلَى بَعْضِ الْأَعْجَمِينَ |
199 |
Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026199.mp3
|
فَقَرَأَهُ عَلَيْهِم مَّا كَانُوا بِهِ مُؤْمِنِينَ |
200 |
Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026200.mp3
|
كَذَلِكَ سَلَكْنَاهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ |
201 |
Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026201.mp3
|
لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ حَتَّى يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ |
202 |
Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026202.mp3
|
فَيَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ |
203 |
Na watasema: Je, tutapewa muhula? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026203.mp3
|
فَيَقُولُوا هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ |
204 |
Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026204.mp3
|
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ |
205 |
Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026205.mp3
|
أَفَرَأَيْتَ إِن مَّتَّعْنَاهُمْ سِنِينَ |
206 |
Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026206.mp3
|
ثُمَّ جَاءهُم مَّا كَانُوا يُوعَدُونَ |
207 |
Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026207.mp3
|
مَا أَغْنَى عَنْهُم مَّا كَانُوا يُمَتَّعُونَ |
208 |
Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji - |
/content/ayah/audio/hudhaify/026208.mp3
|
وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ |
209 |
Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026209.mp3
|
ذِكْرَى وَمَا كُنَّا ظَالِمِينَ |
210 |
Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026210.mp3
|
وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ |
211 |
Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026211.mp3
|
وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ |
212 |
Hakika hao wametengwa na kusikia. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026212.mp3
|
إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ |
213 |
Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026213.mp3
|
فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ |
214 |
Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026214.mp3
|
وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ |
215 |
Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026215.mp3
|
وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ |
216 |
Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026216.mp3
|
فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ |
217 |
Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026217.mp3
|
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ |
218 |
Ambaye anakuona unapo simama, |
/content/ayah/audio/hudhaify/026218.mp3
|
الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ |
219 |
Na mageuko yako kati ya wanao sujudu. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026219.mp3
|
وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ |
220 |
Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026220.mp3
|
إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ |
221 |
Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026221.mp3
|
هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَى مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ |
222 |
Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026222.mp3
|
تَنَزَّلُ عَلَى كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ |
223 |
Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026223.mp3
|
يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ |
224 |
Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026224.mp3
|
وَالشُّعَرَاء يَتَّبِعُهُمُ الْغَاوُونَ |
225 |
Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026225.mp3
|
أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ |
226 |
Na kwamba wao husema wasiyo yatenda? |
/content/ayah/audio/hudhaify/026226.mp3
|
وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ |
227 |
Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. |
/content/ayah/audio/hudhaify/026227.mp3
|
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَذَكَرُوا اللَّهَ كَثِيراً وَانتَصَرُوا مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ |