Al-Hijr

Change Language
Change Surah
Change Recitation

Swahili: Ali Muhsin Al-Barwani

Play All
# Translation Ayah
1 Alif Lam Ra. (A. L. R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha. الَرَ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُّبِينٍ
2 HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu. رُّبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُواْ لَوْ كَانُواْ مُسْلِمِينَ
3 Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua. ذَرْهُمْ يَأْكُلُواْ وَيَتَمَتَّعُواْ وَيُلْهِهِمُ الأَمَلُ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
4 Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu. وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلاَّ وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ
5 Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa. مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ
6 Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu. وَقَالُواْ يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ
7 Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli? لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
8 Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula. مَا نُنَزِّلُ الْمَلائِكَةَ إِلاَّ بِالحَقِّ وَمَا كَانُواْ إِذًا مُّنظَرِينَ
9 Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda. إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
10 Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo. وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الأَوَّلِينَ
11 Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli. وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلاَّ كَانُواْ بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
12 Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu. كَذَلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ
13 Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale. لاَ يُؤْمِنُونَ بِهِ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الأَوَّلِينَ
14 Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda, وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ السَّمَاء فَظَلُّواْ فِيهِ يَعْرُجُونَ
15 Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa. لَقَالُواْ إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ
16 Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia. وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاء بُرُوجًا وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ
17 Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye. وَحَفِظْنَاهَا مِن كُلِّ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ
18 Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kinacho onekana. إِلاَّ مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ مُّبِينٌ
19 Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake. وَالأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْزُونٍ
20 Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku. وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ
21 Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu. وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلاَّ بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ
22 Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka. لَوَاقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاء مَاء فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ
23 Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi. وَإنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ
24 Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari. وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ
25 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi. وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
26 Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. وَلَقَدْ خَلَقْنَا الإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
27 Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto. وَالْجَآنَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ
28 Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلاَئِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
29 Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia. فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُ سَاجِدِينَ
30 Basi Malaika wote pamoja walimsujudia, فَسَجَدَ الْمَلآئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
31 Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu. إِلاَّ إِبْلِيسَ أَبَى أَن يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
32 (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu? قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلاَّ تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
33 Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura. قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
34 (Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ
35 Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo. وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ
36 Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa. قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ
37 (Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ
38 Mpaka siku ya wakati maalumu. إِلَى يَومِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ
39 Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الأَرْضِ وَلأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
40 Ila waja wako walio safika. إِلاَّ عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ
41 Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka. قَالَ هَذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ
42 Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata. إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلاَّ مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ
43 Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ
44 Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa. لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ
45 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
46 (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani. ادْخُلُوهَا بِسَلاَمٍ آمِنِينَ
47 Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana. وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَى سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ
48 Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo. لاَ يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ
49 Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
50 Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu! وَ أَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الأَلِيمَ
51 Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim. وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِ بْراَهِيمَ
52 Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni. إِذْ دَخَلُواْ عَلَيْهِ فَقَالُواْ سَلامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ
53 Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi. قَالُواْ لاَ تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلامٍ عَلِيمٍ
54 Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria? قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَى أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
55 Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa. قَالُواْ بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلاَ تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ
56 Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea? قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلاَّ الضَّآلُّونَ
57 Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe? قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
58 Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu! قَالُواْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَى قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
59 Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote. إِلاَّ آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ
60 Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma. إِلاَّ امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ
61 Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i, فَلَمَّا جَاء آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ
62 Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana. قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
63 Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka. قَالُواْ بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمْتَرُونَ
64 Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli. وَأَتَيْنَاكَ بَالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ
65 Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa. فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلاَ يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُواْ حَيْثُ تُؤْمَرُونَ
66 Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali. وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَلِكَ الأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَؤُلاء مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ
67 Na wakaja watu wa mji ule nao furahani. وَجَاء أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ
68 Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe. قَالَ إِنَّ هَؤُلاء ضَيْفِي فَلاَ تَفْضَحُونِ
69 Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi. وَاتَّقُوا اللّهَ وَلاَ تُخْزُونِ
70 Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote? قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ
71 Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji. قَالَ هَؤُلاء بَنَاتِي إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ
72 Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo. لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ
73 Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa. فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ
74 Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni. فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ
75 Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi. إِنَّ فِي ذَلِكَ لآيَاتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ
76 Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa. وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقيمٍ
77 Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini. إِنَّ فِي ذَلِكَ لآيَةً لِّلْمُؤمِنِينَ
78 Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu. وَإِن كَانَ أَصْحَابُ الأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ
79 Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi. فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ
80 Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume. وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ
81 Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza. وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُواْ عَنْهَا مُعْرِضِينَ
82 Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani. وَكَانُواْ يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا آمِنِينَ
83 Basi ukelele ukawatwaa asubuhi. فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ
84 Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma. فَمَا أَغْنَى عَنْهُم مَّا كَانُواْ يَكْسِبُونَ
85 Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri. وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلاَّ بِالْحَقِّ وَإِنَّ السَّاعَةَ لآتِيَةٌ فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ
86 Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi. إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلاَّقُ الْعَلِيمُ
87 Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu. وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِّنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ
88 Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini. لاَ تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَى مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلاَ تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ
89 Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha. وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ
90 Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa, كَمَا أَنزَلْنَا عَلَى المُقْتَسِمِينَ
91 Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande. الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ
92 Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote, فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِيْنَ
93 Kwa waliyo kuwa wakiyatenda. عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
94 Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina. فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
95 Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli. إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ
96 Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua! الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللّهِ إِلـهًا آخَرَ فَسَوْفَ يَعْمَلُونَ
97 Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo. وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
98 Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia. فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ
99 Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini. وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ
;